Wagalatia 4:27
Galatians 4:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana imeandikwa: “Furahi, ewe mwanamke tasa, wewe usiyezaa; paza sauti, na kuimba kwa furaha, wewe usiyepatwa na utungu wa kuzaa; kwa maana watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi kuliko wa mwanamke mwenye mume.”
Galatians 4:27 in English
Galatians 4:27 · Berean Standard Bible
For it is written: “Rejoice, O barren woman, who bears no children; break forth and cry aloud, you who have never travailed; because more are the children of the desolate woman than of her who has a husband.”*
Context
25Basi Hagari anawakilisha Mlima Sinai ulioko Arabuni, na unafanana na Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake. 26Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, nayo ndiye mama yetu. 27Kwa maana imeandikwa:
“Furahi, ewe mwanamke tasa,
wewe usiyezaa;
paza sauti, na kuimba kwa furaha,
wewe usiyepatwa na utungu wa kuzaa;
kwa maana watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi
kuliko wa mwanamke mwenye mume.” 28Basi, sisi ndugu zangu, ni kama Isaki, tu watoto wa ahadi. 29Lakini, kama vile ilivyokuwa siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomchokoza yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo hata sasa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.