Wagalatia 4:26
Galatians 4:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, nayo ndiye mama yetu.
Galatians 4:26 in English
Galatians 4:26 · Berean Standard Bible
But the Jerusalem above is free, and she is our mother.
Context
24Mambo haya yanaweza kuchukuliwa kama mfano. Kwa maana hao wanawake wawili ni mfano wa maagano mawili: Agano la kwanza, ni lile lililofanyika katika Mlima Sinai, lizaalo watoto wa utumwa. Hili ndilo huyo Hagari. 25Basi Hagari anawakilisha Mlima Sinai ulioko Arabuni, na unafanana na Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake. 26Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, nayo ndiye mama yetu. 27Kwa maana imeandikwa:
“Furahi, ewe mwanamke tasa,
wewe usiyezaa;
paza sauti, na kuimba kwa furaha,
wewe usiyepatwa na utungu wa kuzaa;
kwa maana watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi
kuliko wa mwanamke mwenye mume.” 28Basi, sisi ndugu zangu, ni kama Isaki, tu watoto wa ahadi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.