Native Bible

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Niliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa Bwana. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa Bwana, Mungu wa baba zenu.

Ezra 8:28 in English

Ezra 8:28 · Berean Standard Bible

Then I told them, “You are holy to the LORD, and these articles are holy. The silver and gold are a freewill offering to the LORD, the God of your fathers.

Context

26Niliwapimia talanta 650* za fedha, vifaa vingine vya fedha vya uzito wa talanta mia moja,* talanta mia moja za dhahabu, 27mabakuli ishirini ya dhahabu ya thamani ya darkoni elfu moja,* na vyombo viwili vya shaba iliyosuguliwa, ya thamani kama dhahabu. 28Niliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa Bwana. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa Bwana, Mungu wa baba zenu. 29Vilindeni kwa uangalifu mpaka mtakapovipima ndani ya vyumba vya nyumba ya Bwana katika Yerusalemu mbele ya makuhani, viongozi na Walawi pamoja na wakuu wa jamaa za Israeli.” 30Ndipo makuhani na Walawi wakapokea fedha, dhahabu na vyombo vilivyowekwa wakfu ambavyo vilipimwa na kupelekwa katika nyumba ya Mungu wetu mjini Yerusalemu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.