Native Bible

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Niliwapimia talanta 650* za fedha, vifaa vingine vya fedha vya uzito wa talanta mia moja,* talanta mia moja za dhahabu,

Ezra 8:26 in English

Ezra 8:26 · Berean Standard Bible

I weighed out into their hands 650 talents of silver,* articles of silver weighing 100 talents,* 100 talents of gold,*

Context

24Kisha niliwatenga viongozi wa makuhani kumi na wawili, pamoja na Sherebia, Hashabia na ndugu zao kumi, 25nami nikawapimia fedha, dhahabu na vifaa ambavyo mfalme, washauri wake, maafisa wake na Israeli wote waliokuwepo walikuwa wamevitoa sadaka kwa ajili ya nyumba ya Mungu wetu. 26Niliwapimia talanta 650* za fedha, vifaa vingine vya fedha vya uzito wa talanta mia moja,* talanta mia moja za dhahabu, 27mabakuli ishirini ya dhahabu ya thamani ya darkoni elfu moja,* na vyombo viwili vya shaba iliyosuguliwa, ya thamani kama dhahabu. 28Niliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa Bwana. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa Bwana, Mungu wa baba zenu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.