Native Bible

Ezekiel 47:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akaniuliza, “Je, mwanadamu, unaona hili?” Kisha akanirudisha mpaka kwenye ukingo wa huo mto.

Ezekiel 47:6 in English

Ezekiel 47:6 · Berean Standard Bible

“Son of man, do you see this?” he asked. Then he led me back to the bank of the river.

Context

4Akapima dhiraa 1,000 nyingine na kunipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika magotini. Akapima dhiraa nyingine 1,000 na kunipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika kiunoni. 5Akapima tena dhiraa 1,000 nyingine, lakini wakati huu yalikuwa mto ambao sikuweza kuvuka, kwa kuwa maji yalikuwa na kina kirefu ambacho ni cha kuogelea, mto ambao hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuvuka. 6Akaniuliza, “Je, mwanadamu, unaona hili?” Kisha akanirudisha mpaka kwenye ukingo wa huo mto. 7Nilipofika pale, nikaona idadi kubwa ya miti kila upande wa ule mto. 8Akaniambia, “Haya maji yanatiririka kuelekea nchi ya mashariki na kushuka mpaka Araba,* ambapo huingia Baharini. Yanapomwagikia kwenye hiyo Bahari,* maji yaliyoko humo huponywa na kuwa safi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.