Ezekieli 47:7
Ezekiel 47:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nilipofika pale, nikaona idadi kubwa ya miti kila upande wa ule mto.
Ezekiel 47:7 in English
Ezekiel 47:7 · Berean Standard Bible
When I arrived, I saw a great number of trees along both banks of the river.
Context
5Akapima tena dhiraa 1,000 nyingine, lakini wakati huu yalikuwa mto ambao sikuweza kuvuka, kwa kuwa maji yalikuwa na kina kirefu ambacho ni cha kuogelea, mto ambao hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuvuka. 6Akaniuliza, “Je, mwanadamu, unaona hili?”
Kisha akanirudisha mpaka kwenye ukingo wa huo mto. 7Nilipofika pale, nikaona idadi kubwa ya miti kila upande wa ule mto. 8Akaniambia, “Haya maji yanatiririka kuelekea nchi ya mashariki na kushuka mpaka Araba,* ambapo huingia Baharini. Yanapomwagikia kwenye hiyo Bahari,* maji yaliyoko humo huponywa na kuwa safi. 9Popote mto huu uendapo kila kiumbe hai kinachoyaparamia hayo maji kitaishi, nako kutakuwa na samaki wengi mno, mara maji haya yafikapo huko. Maji hayo yatakuwa hai na kila kitu kitakachoishi kule mto uendako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.