Ezekieli 47:5
Ezekiel 47:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akapima tena dhiraa 1,000 nyingine, lakini wakati huu yalikuwa mto ambao sikuweza kuvuka, kwa kuwa maji yalikuwa na kina kirefu ambacho ni cha kuogelea, mto ambao hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuvuka.
Ezekiel 47:5 in English
Ezekiel 47:5 · Berean Standard Bible
Once again he measured off a thousand cubits, but now it was a river that I could not cross, because the water had risen and was deep enough for swimming—a river that could not be crossed on foot.
Context
3Mtu yule alipokwenda upande wa mashariki akiwa na kamba ya kupimia mkononi mwake, akapima dhiraa 1,000* kisha akanipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika kwenye vifundo vya miguu. 4Akapima dhiraa 1,000 nyingine na kunipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika magotini. Akapima dhiraa nyingine 1,000 na kunipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika kiunoni. 5Akapima tena dhiraa 1,000 nyingine, lakini wakati huu yalikuwa mto ambao sikuweza kuvuka, kwa kuwa maji yalikuwa na kina kirefu ambacho ni cha kuogelea, mto ambao hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuvuka. 6Akaniuliza, “Je, mwanadamu, unaona hili?”
Kisha akanirudisha mpaka kwenye ukingo wa huo mto. 7Nilipofika pale, nikaona idadi kubwa ya miti kila upande wa ule mto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.