Ezekieli 43:4
Ezekiel 43:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utukufu wa Bwana ukaingia hekaluni kwa kupitia lango linaloelekea upande wa mashariki.
Ezekiel 43:4 in English
Ezekiel 43:4 · Berean Standard Bible
and the glory of the LORD entered the temple through the gate facing east.
Context
2nami nikaona utukufu wa Mungu wa Israeli ukija kutoka upande wa mashariki. Sauti yake ilikuwa kama ya ngurumo ya maji yaendayo kasi, nayo nchi ikangʼaa kwa utukufu wake. 3Maono niliyoyaona yalikuwa kama maono yale niliyokuwa nimeyaona wakati Mungu alipokuja kuangamiza mji na kama maono niliyokuwa nimeyaona kando ya Mto wa Kebari, nami nikaanguka kifudifudi. 4Utukufu wa Bwana ukaingia hekaluni kwa kupitia lango linaloelekea upande wa mashariki. 5Kisha Roho akanichukua na kunileta katika ule ua wa ndani, nao utukufu wa Bwana ulilijaza Hekalu. 6Wakati yule mtu akiwa amesimama kando yangu, nilisikia mtu mmoja akisema nami kutoka ndani ya Hekalu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.