Native Bible

Ezekiel 43:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha Roho akanichukua na kunileta katika ule ua wa ndani, nao utukufu wa Bwana ulilijaza Hekalu.

Ezekiel 43:5 in English

Ezekiel 43:5 · Berean Standard Bible

Then the Spirit lifted me up and brought me into the inner court, and the glory of the LORD filled the temple.

Context

3Maono niliyoyaona yalikuwa kama maono yale niliyokuwa nimeyaona wakati Mungu alipokuja kuangamiza mji na kama maono niliyokuwa nimeyaona kando ya Mto wa Kebari, nami nikaanguka kifudifudi. 4Utukufu wa Bwana ukaingia hekaluni kwa kupitia lango linaloelekea upande wa mashariki. 5Kisha Roho akanichukua na kunileta katika ule ua wa ndani, nao utukufu wa Bwana ulilijaza Hekalu. 6Wakati yule mtu akiwa amesimama kando yangu, nilisikia mtu mmoja akisema nami kutoka ndani ya Hekalu. 7Akasema, “Mwanadamu, hapa ni mahali pa kiti changu cha enzi na mahali pa kuweka nyayo za miguu yangu. Hapa ndipo nitakapoishi miongoni mwa Waisraeli milele. Kamwe nyumba ya Israeli hawatalinajisi tena Jina langu takatifu, yaani, wao wala wafalme wao, kwa ukahaba wao na kwa sanamu zao zisizokuwa na uhai za wafalme wao katika mahali pao pa juu pa kuabudia miungu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.