Native Bible

Ezekiel 43:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

nami nikaona utukufu wa Mungu wa Israeli ukija kutoka upande wa mashariki. Sauti yake ilikuwa kama ya ngurumo ya maji yaendayo kasi, nayo nchi ikangʼaa kwa utukufu wake.

Ezekiel 43:2 in English

Ezekiel 43:2 · Berean Standard Bible

and I saw the glory of the God of Israel coming from the east. His voice was like the roar of many waters, and the earth shone with His glory.

Context

1Kisha yule mtu akanileta kwenye lango linaloelekea upande wa mashariki, 2nami nikaona utukufu wa Mungu wa Israeli ukija kutoka upande wa mashariki. Sauti yake ilikuwa kama ya ngurumo ya maji yaendayo kasi, nayo nchi ikangʼaa kwa utukufu wake. 3Maono niliyoyaona yalikuwa kama maono yale niliyokuwa nimeyaona wakati Mungu alipokuja kuangamiza mji na kama maono niliyokuwa nimeyaona kando ya Mto wa Kebari, nami nikaanguka kifudifudi. 4Utukufu wa Bwana ukaingia hekaluni kwa kupitia lango linaloelekea upande wa mashariki.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.