Native Bible

Ezekiel 43:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha yule mtu akanileta kwenye lango linaloelekea upande wa mashariki,

Ezekiel 43:1 in English

Ezekiel 43:1 · Berean Standard Bible

Then the man brought me back to the gate that faces east,

Context

1Kisha yule mtu akanileta kwenye lango linaloelekea upande wa mashariki, 2nami nikaona utukufu wa Mungu wa Israeli ukija kutoka upande wa mashariki. Sauti yake ilikuwa kama ya ngurumo ya maji yaendayo kasi, nayo nchi ikangʼaa kwa utukufu wake. 3Maono niliyoyaona yalikuwa kama maono yale niliyokuwa nimeyaona wakati Mungu alipokuja kuangamiza mji na kama maono niliyokuwa nimeyaona kando ya Mto wa Kebari, nami nikaanguka kifudifudi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.