Ezekieli 24:8
Ezekiel 24:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kuchochea ghadhabu na kulipiza kisasi, nimemwaga damu yake juu ya mwamba ulio wazi, ili isifunikwe.
Ezekiel 24:8 in English
Ezekiel 24:8 · Berean Standard Bible
In order to stir up wrath and take vengeance, I have placed her blood on the bare rock, so that it would not be covered.’
Context
6“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Ole wa mji umwagao damu,
ole wa sufuria ambayo sasa
ina ukoko ndani yake,
ambayo ukoko wake hautoki.
Kipakue kipande baada ya kipande,
bila kuvipigia kura. 7“ ‘Kwa kuwa damu aliyoimwaga ipo katikati yake:
huyo mwanamke aliimwaga
juu ya mwamba ulio wazi;
hakuimwaga kwenye ardhi,
ambako vumbi lingeifunika. 8Kuchochea ghadhabu na kulipiza kisasi,
nimemwaga damu yake
juu ya mwamba ulio wazi,
ili isifunikwe. 9“ ‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Ole wa mji umwagao damu!
Mimi nami nitalundikia kuni nyingi. 10Kwa hiyo lundika kuni
na uwashe moto.
Pika hiyo nyama vizuri,
changanya viungo ndani yake,
na uiache mifupa iungue kwenye moto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.