Ezekieli 21:15
Ezekiel 21:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ili mioyo ipate kuyeyuka na wanaouawa wawe wengi, nimeweka upanga wa kuchinja kwenye malango yao yote. Lo! Umetengenezwa umetemete kama umeme wa radi, umeshikwa kwa ajili ya kuua.
Ezekiel 21:15 in English
Ezekiel 21:15 · Berean Standard Bible
So that their hearts may melt and many may stumble, I have appointed at all their gates a sword for slaughter. Yes, it is ready to flash like lightning; it is drawn for slaughter.
Context
13“ ‘Kwa maana upanga huu umejaribiwa na kuhakikishwa, itakuwaje basi fimbo ya ufalme ya Yuda inayoudharau kama haitakuwepo tena, bali itakuwa imeondolewa kabisa? asema Bwana Mwenyezi.’ 14“Hivyo basi, mwanadamu, tabiri
na ukapige makofi.
Upanga wako na upige mara mbili,
naam, hata mara tatu.
Ni upanga wa kuchinja,
upanga wa mauaji makuu,
ukiwashambulia kutoka kila upande. 15Ili mioyo ipate kuyeyuka
na wanaouawa wawe wengi,
nimeweka upanga wa kuchinja
kwenye malango yao yote.
Lo! Umetengenezwa
umetemete kama umeme wa radi,
umeshikwa kwa ajili ya kuua. 16Ee upanga, kata upande wa kuume,
kisha upande wa kushoto,
mahali popote makali yako
yatakapoelekezwa. 17Mimi nami nitapiga makofi,
nayo ghadhabu yangu itapungua.
Mimi Bwana nimesema.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.