Ezekieli 21:17
Ezekiel 21:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mimi nami nitapiga makofi, nayo ghadhabu yangu itapungua. Mimi Bwana nimesema.”
Ezekiel 21:17 in English
Ezekiel 21:17 · Berean Standard Bible
I too will strike My hands together, and I will satisfy My wrath.’ I, the LORD, have spoken.”
Context
15Ili mioyo ipate kuyeyuka
na wanaouawa wawe wengi,
nimeweka upanga wa kuchinja
kwenye malango yao yote.
Lo! Umetengenezwa
umetemete kama umeme wa radi,
umeshikwa kwa ajili ya kuua. 16Ee upanga, kata upande wa kuume,
kisha upande wa kushoto,
mahali popote makali yako
yatakapoelekezwa. 17Mimi nami nitapiga makofi,
nayo ghadhabu yangu itapungua.
Mimi Bwana nimesema.” 18Neno la Bwana likanijia kusema: 19“Mwanadamu, weka alama njia mbili ambazo upanga wa mfalme wa Babeli utapitia, njia hizo zikianzia katika nchi hiyo hiyo. Weka kibao pale ambapo njia zinagawanyika kuelekea mjini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.