Ezekieli 18:8
Ezekiel 18:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakopeshi kwa riba wala hajipatii faida ya ziada. Huuzuia mkono wake usifanye mabaya, naye huhukumu kwa haki kati ya mtu na mtu.
Ezekiel 18:8 in English
Ezekiel 18:8 · Berean Standard Bible
He does not engage in usury or take excess interest, but he withholds his hand from iniquity and executes true justice between men.
Context
6Hakula katika mahali pa ibada za miungu
kwenye milima
wala hakuziinulia macho sanamu
za nyumba ya Israeli.
Hakumtia unajisi mke wa jirani yake,
wala hakukutana kimwili na mwanamke
wakati wa siku zake za hedhi. 7Hamwonei mtu yeyote,
bali hurudisha kilichowekwa rehani kwake.
Hanyangʼanyi, bali huwapa wenye njaa chakula chake
na huwapa nguo walio uchi. 8Hakopeshi kwa riba
wala hajipatii faida ya ziada.
Huuzuia mkono wake usifanye mabaya,
naye huhukumu kwa haki kati ya mtu na mtu. 9Huzifuata amri zangu
na kuzishika sheria zangu kwa uaminifu.
Huyo mtu ni mwenye haki;
hakika ataishi,
asema Bwana Mwenyezi. 10“Aweza kuwa ana mwana jeuri, amwagaye damu au atendaye mojawapo ya mambo haya
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.