Ezekieli 18:6
Ezekiel 18:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakula katika mahali pa ibada za miungu kwenye milima wala hakuziinulia macho sanamu za nyumba ya Israeli. Hakumtia unajisi mke wa jirani yake, wala hakukutana kimwili na mwanamke wakati wa siku zake za hedhi.
Ezekiel 18:6 in English
Ezekiel 18:6 · Berean Standard Bible
He does not eat at the mountain or look to the idols of the house of Israel. He does not defile his neighbor’s wife or approach a woman during her period.
Context
4Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. 5“Mtu aweza kuwa ni mwenye haki
atendaye yaliyo haki na sawa. 6Hakula katika mahali pa ibada za miungu
kwenye milima
wala hakuziinulia macho sanamu
za nyumba ya Israeli.
Hakumtia unajisi mke wa jirani yake,
wala hakukutana kimwili na mwanamke
wakati wa siku zake za hedhi. 7Hamwonei mtu yeyote,
bali hurudisha kilichowekwa rehani kwake.
Hanyangʼanyi, bali huwapa wenye njaa chakula chake
na huwapa nguo walio uchi. 8Hakopeshi kwa riba
wala hajipatii faida ya ziada.
Huuzuia mkono wake usifanye mabaya,
naye huhukumu kwa haki kati ya mtu na mtu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.