Native Bible

Exodus 18:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baba mkwe wa Mose akamjibu, “Unachofanya sio kizuri.

Exodus 18:17 in English

Exodus 18:17 · Berean Standard Bible

But Moses’ father-in-law said to him, “What you are doing is not good.

Context

15Mose akamjibu, “Kwa sababu watu wananijia kutaka mapenzi ya Mungu. 16Kila wakiwa na shauri huletwa kwangu, nami huamua kati ya mtu na mwenzake na kuwajulisha juu ya amri na sheria za Mungu.” 17Baba mkwe wa Mose akamjibu, “Unachofanya sio kizuri. 18Wewe pamoja na watu hawa wanaokujia mtajichosha bure. Kazi ni nzito sana kwako, huwezi kuibeba mwenyewe. 19Sasa nisikilize mimi, nitakupa shauri, naye Mungu na awe pamoja nawe. Yapasa wewe uwe mwakilishi wa watu mbele za Mungu na ulete mashauri yao kwake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.