Native Bible

Exodus 18:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mose akamjibu, “Kwa sababu watu wananijia kutaka mapenzi ya Mungu.

Exodus 18:15 in English

Exodus 18:15 · Berean Standard Bible

“Because the people come to me to inquire of God,” Moses replied.

Context

13Siku iliyofuata, Mose akachukua nafasi yake kama hakimu wa watu, nao wakasimama kumzunguka kuanzia asubuhi hadi jioni. 14Baba mkwe wake alipoona yote Mose anayowafanyia watu, akasema, “Ni nini hiki unachowafanyia watu? Kwa nini wewe unakuwa mwamuzi wa watu hawa peke yako, wakati watu hawa wamesimama wakikuzunguka tangu asubuhi mpaka jioni?” 15Mose akamjibu, “Kwa sababu watu wananijia kutaka mapenzi ya Mungu. 16Kila wakiwa na shauri huletwa kwangu, nami huamua kati ya mtu na mwenzake na kuwajulisha juu ya amri na sheria za Mungu.” 17Baba mkwe wa Mose akamjibu, “Unachofanya sio kizuri.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.