Waefeso 6:11
Ephesians 6:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi.
Ephesians 6:11 in English
Ephesians 6:11 · Berean Standard Bible
Put on the full armor of God, so that you can make your stand against the devil’s schemes.
Context
9Nanyi mabwana, watendeeni watumwa wenu kwa jinsi iyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua ya kwamba yeye aliye Bwana wenu na Bwana wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo. 10Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi. 12Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.