Mhubiri 4:3
Ecclesiastes 4:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini aliye bora kuliko hao wawili ni yule ambaye hajazaliwa bado, ambaye hajaona ule uovu unaofanyika chini ya jua.
Ecclesiastes 4:3 in English
Ecclesiastes 4:3 · Berean Standard Bible
But better than both is he who has not yet existed, who has not seen the evil that is done under the sun.
Context
1Nikatazama tena nikaona uonevu wote uliokuwa unafanyika chini ya jua:
Nikaona machozi ya walioonewa,
wala hawana wa kuwafariji;
uwezo ulikuwa upande wa wale wanaowaonea,
wala hawana wa kuwafariji. 2Nami nikasema kwamba wafu,
waliokwisha kufa,
wana furaha kuliko watu walio hai,
ambao bado wanaishi. 3Lakini aliye bora kuliko hao wawili
ni yule ambaye hajazaliwa bado,
ambaye hajaona ule uovu
unaofanyika chini ya jua. 4Tena nikaona kuwa kazi zote na mafanikio yote huchipuka kutokana na wivu wa mtu kwa jirani yake. Hili nalo ni ubatili, ni kukimbiza upepo. 5Mpumbavu hukunja mikono yake
na kujiangamiza mwenyewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.