Mhubiri 2:4
Ecclesiastes 2:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nikafanya miradi mikubwa: Nikajijengea majumba na kulima mashamba ya mizabibu.
Ecclesiastes 2:4 in English
Ecclesiastes 2:4 · Berean Standard Bible
I expanded my pursuits. I built houses and planted vineyards for myself.
Context
2Nikasema, “Kicheko nacho ni upumbavu. Nayo matokeo ya anasa ni nini?” 3Nikajaribu kujifurahisha kwa mvinyo na kukumbatia upumbavu, huku bado akili yangu inaniongoza kwa hekima. Nilitaka kuona ni lipi bora watu wafanye kwa siku chache wanazoishi chini ya mbingu. 4Nikafanya miradi mikubwa: Nikajijengea majumba na kulima mashamba ya mizabibu. 5Nikatengeneza bustani na viwanja vya starehe nikaotesha huko kila aina ya miti ya matunda. 6Nikajenga mabwawa ya kukusanya maji ya kunyweshea hii miti iliyokuwa inastawi vizuri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.