Native Bible

Ecclesiastes 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nikajaribu kujifurahisha kwa mvinyo na kukumbatia upumbavu, huku bado akili yangu inaniongoza kwa hekima. Nilitaka kuona ni lipi bora watu wafanye kwa siku chache wanazoishi chini ya mbingu.

Ecclesiastes 2:3 in English

Ecclesiastes 2:3 · Berean Standard Bible

I sought to cheer my body with wine and to embrace folly—my mind still guiding me with wisdom—until I could see what was worthwhile for men to do under heaven during the few days of their lives.

Context

1Nikafikiri moyoni mwangu, “Haya basi, nitakujaribu kwa anasa nione ni lipi lililo jema.” Lakini hilo nalo likaonekana ni ubatili. 2Nikasema, “Kicheko nacho ni upumbavu. Nayo matokeo ya anasa ni nini?” 3Nikajaribu kujifurahisha kwa mvinyo na kukumbatia upumbavu, huku bado akili yangu inaniongoza kwa hekima. Nilitaka kuona ni lipi bora watu wafanye kwa siku chache wanazoishi chini ya mbingu. 4Nikafanya miradi mikubwa: Nikajijengea majumba na kulima mashamba ya mizabibu. 5Nikatengeneza bustani na viwanja vya starehe nikaotesha huko kila aina ya miti ya matunda.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.