Mhubiri 2:5
Ecclesiastes 2:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nikatengeneza bustani na viwanja vya starehe nikaotesha huko kila aina ya miti ya matunda.
Ecclesiastes 2:5 in English
Ecclesiastes 2:5 · Berean Standard Bible
I made gardens and parks for myself, where I planted all kinds of fruit trees.
Context
3Nikajaribu kujifurahisha kwa mvinyo na kukumbatia upumbavu, huku bado akili yangu inaniongoza kwa hekima. Nilitaka kuona ni lipi bora watu wafanye kwa siku chache wanazoishi chini ya mbingu. 4Nikafanya miradi mikubwa: Nikajijengea majumba na kulima mashamba ya mizabibu. 5Nikatengeneza bustani na viwanja vya starehe nikaotesha huko kila aina ya miti ya matunda. 6Nikajenga mabwawa ya kukusanya maji ya kunyweshea hii miti iliyokuwa inastawi vizuri. 7Nikanunua watumwa wa kiume na wa kike na watumwa wengine walizaliwa nyumbani mwangu. Pia nilikuwa na makundi ya ngʼombe, kondoo na mbuzi kuliko mtu yeyote aliyewahi kuishi Yerusalemu kabla yangu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.