Native Bible

Ecclesiastes 11:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wape sehemu watu saba, naam hata wanane, kwa maana hujui ni baa gani litakalokuwa juu ya nchi.

Ecclesiastes 11:2 in English

Ecclesiastes 11:2 · Berean Standard Bible

Divide your portion among seven, or even eight, for you do not know what disaster may befall the land.

Context

1Tupa mkate wako juu ya maji, kwa maana baada ya siku nyingi utaupata tena. 2Wape sehemu watu saba, naam hata wanane, kwa maana hujui ni baa gani litakalokuwa juu ya nchi. 3Kama mawingu yamejaa maji, hunyesha mvua juu ya nchi. Kama mti ukianguka kuelekea kusini au kuelekea kaskazini, mahali ulipoangukia, hapo ndipo utakapolala. 4Yeyote atazamaye upepo hatapanda, yeyote aangaliaye mawingu hatavuna.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.