Native Bible

Ecclesiastes 11:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yeyote atazamaye upepo hatapanda, yeyote aangaliaye mawingu hatavuna.

Ecclesiastes 11:4 in English

Ecclesiastes 11:4 · Berean Standard Bible

He who watches the wind will fail to sow, and he who observes the clouds will fail to reap.

Context

2Wape sehemu watu saba, naam hata wanane, kwa maana hujui ni baa gani litakalokuwa juu ya nchi. 3Kama mawingu yamejaa maji, hunyesha mvua juu ya nchi. Kama mti ukianguka kuelekea kusini au kuelekea kaskazini, mahali ulipoangukia, hapo ndipo utakapolala. 4Yeyote atazamaye upepo hatapanda, yeyote aangaliaye mawingu hatavuna. 5Kama vile usivyofahamu njia ya upepo, au jinsi mwili uumbwavyo ndani ya tumbo la mama, vivyo hivyo huwezi kufahamu kazi ya Mungu, Muumba wa vitu vyote. 6Panda mbegu yako asubuhi, nako jioni usiruhusu mikono yako ilegee, kwa maana hujui ni ipi itakayofanikiwa, kwamba ni hii au ni ile, au kwamba zote zitafanikiwa sawasawa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.