Kumbukumbu 8:7
Deuteronomy 8:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa kuwa Bwana Mungu wenu anawaleta katika nchi nzuri, nchi yenye vijito na mabwawa ya maji, yenye chemchemi zinazotiririka mabondeni na katika vilima;
Deuteronomy 8:7 in English
Deuteronomy 8:7 · Berean Standard Bible
For the LORD your God is bringing you into a good land, a land of brooks and fountains and springs that flow through the valleys and hills;
Context
5Mjue basi ndani ya mioyo yenu kama mtu anavyomwadibisha mwanawe, ndivyo Bwana Mungu wako atawaadibisha ninyi. 6Shikeni maagizo ya Bwana Mungu wenu mtembee katika njia zake na kumheshimu. 7Kwa kuwa Bwana Mungu wenu anawaleta katika nchi nzuri, nchi yenye vijito na mabwawa ya maji, yenye chemchemi zinazotiririka mabondeni na katika vilima; 8nchi yenye ngano na shayiri, mizabibu na mitini, mikomamanga, mafuta ya zeituni na asali; 9nchi ambayo chakula hakitapungua na hamtakosa chochote; nchi ambayo miamba yake ni chuma na mnaweza kuchimba shaba kutoka kwenye vilima.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.