Kumbukumbu 33:7
Deuteronomy 33:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akasema hili kuhusu Yuda: “Ee Bwana, sikia kilio cha Yuda, mlete kwa watu wake. Kwa mikono yake mwenyewe hujitetea. Naam, uwe msaada wake dhidi ya adui zake!”
Deuteronomy 33:7 in English
Deuteronomy 33:7 · Berean Standard Bible
And concerning Judah he said: “O LORD, hear the cry of Judah and bring him to his people. With his own hands he defends his cause, but may You be a help against his foes.”
Context
5Alikuwa mfalme juu ya Yeshuruni*
wakati viongozi wa watu walipokusanyika,
pamoja na makabila ya Israeli. 6“Reubeni na aishi, asife,
wala watu wake wasiwe wachache.” 7Akasema hili kuhusu Yuda:
“Ee Bwana, sikia kilio cha Yuda,
mlete kwa watu wake.
Kwa mikono yake mwenyewe hujitetea.
Naam, uwe msaada wake
dhidi ya adui zake!” 8Kuhusu Lawi alisema:
“Thumimu yako na Urimu* yako ulimpa,
mtu yule uliyemfadhili.
Ulimjaribu huko Masa
na kushindana naye
kwenye maji ya Meriba. 9Alinena hivi kuhusu baba yake na mama yake,
‘Mimi siwahitaji kamwe.’
Akawasahau jamaa zake,
asiwatambue hata watoto wake,
lakini akaliangalia neno lako
na kulilinda Agano lako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.