Native Bible

Deuteronomy 33:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kuhusu Lawi alisema: “Thumimu yako na Urimu* yako ulimpa, mtu yule uliyemfadhili. Ulimjaribu huko Masa na kushindana naye kwenye maji ya Meriba.

Deuteronomy 33:8 in English

Deuteronomy 33:8 · Berean Standard Bible

Concerning Levi he said: “Give Your Thummim to Levi and Your Urim to Your godly one,* whom You tested at Massah * and contested at the waters of Meribah.*

Context

6“Reubeni na aishi, asife, wala watu wake wasiwe wachache.” 7Akasema hili kuhusu Yuda: “Ee Bwana, sikia kilio cha Yuda, mlete kwa watu wake. Kwa mikono yake mwenyewe hujitetea. Naam, uwe msaada wake dhidi ya adui zake!” 8Kuhusu Lawi alisema: “Thumimu yako na Urimu* yako ulimpa, mtu yule uliyemfadhili. Ulimjaribu huko Masa na kushindana naye kwenye maji ya Meriba. 9Alinena hivi kuhusu baba yake na mama yake, ‘Mimi siwahitaji kamwe.’ Akawasahau jamaa zake, asiwatambue hata watoto wake, lakini akaliangalia neno lako na kulilinda Agano lako. 10Humfundisha Yakobo mausia yako na Israeli sheria yako. Hufukiza uvumba mbele zako na sadaka nzima za kuteketezwa juu ya madhabahu yako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.