Kumbukumbu 33:3
Deuteronomy 33:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakika ni wewe ambaye huwapenda watu, watakatifu wako wote wamo mkononi mwako. Miguuni pako wote wanasujudu na kutoka kwako wanapokea mafundisho,
Deuteronomy 33:3 in English
Deuteronomy 33:3 · Berean Standard Bible
Surely You love the people; all the holy ones are in Your hand, and they sit down at Your feet;* each receives Your words—
Context
1Hii ndiyo baraka Mose mtu wa Mungu aliyotamka kwa Waisraeli kabla ya kifo chake. 2Alisema:
“Bwana alikuja kutoka Mlima Sinai,
akachomoza kama jua juu yao
kutoka Mlima Seiri,
akaangaza kutoka Mlima Parani.
Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu
kutoka kusini,
kutoka materemko ya mlima wake. 3Hakika ni wewe ambaye huwapenda watu,
watakatifu wako wote wamo mkononi mwako.
Miguuni pako wote wanasujudu
na kutoka kwako wanapokea mafundisho, 4sheria ile Mose aliyotupa sisi,
tulio milki ya kusanyiko la Yakobo. 5Alikuwa mfalme juu ya Yeshuruni*
wakati viongozi wa watu walipokusanyika,
pamoja na makabila ya Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.