Native Bible

Deuteronomy 28:44 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yeye atakukopesha, lakini wewe hutamkopesha. Yeye atakuwa kichwa, lakini wewe utakuwa mkia.

Deuteronomy 28:44 in English

Deuteronomy 28:44 · Berean Standard Bible

He will lend to you, but you will not lend to him. He will be the head, and you will be the tail.

Context

42Makundi ya nzige yatavamia miti yako yote na mazao ya nchi yako. 43Mgeni anayeishi miongoni mwako atainuka juu zaidi na zaidi kuliko wewe, lakini wewe utashuka chini zaidi na zaidi. 44Yeye atakukopesha, lakini wewe hutamkopesha. Yeye atakuwa kichwa, lakini wewe utakuwa mkia. 45Laana hizi zote zitakuja juu yako. Zitakufuatia na kukupata mpaka uangamizwe, kwa sababu hukumtii Bwana Mungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake aliyokupa. 46Zitakuwa ishara na ajabu kwako na kwa wazao wako milele.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.