Kumbukumbu 28:39
Deuteronomy 28:39 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utapanda mashamba ya mizabibu na kuyapalilia, lakini hutakunywa divai yake wala hutakusanya zabibu, kwa sababu wadudu watazila.
Deuteronomy 28:39 in English
Deuteronomy 28:39 · Berean Standard Bible
You will plant and cultivate vineyards, but will neither drink the wine nor gather the grapes, because worms will eat them.
Context
37Utakuwa kitu cha kuchukiza, tena kitu cha kudharauliwa na kudhihakiwa kwa mataifa yote huko Bwana atakakokupeleka. 38Utapanda mbegu nyingi katika shamba lakini utavuna haba, kwa sababu nzige watazila. 39Utapanda mashamba ya mizabibu na kuyapalilia, lakini hutakunywa divai yake wala hutakusanya zabibu, kwa sababu wadudu watazila. 40Utakuwa na mizeituni katika nchi yako yote, lakini hutatumia hayo mafuta yake, kwa sababu zeituni zitapukutika. 41Utakuwa na wana na binti lakini hawatakuwa nawe, kwa sababu watachukuliwa mateka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.