Native Bible

Deuteronomy 28:40 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Utakuwa na mizeituni katika nchi yako yote, lakini hutatumia hayo mafuta yake, kwa sababu zeituni zitapukutika.

Deuteronomy 28:40 in English

Deuteronomy 28:40 · Berean Standard Bible

You will have olive trees throughout your territory but will never anoint yourself with oil, because the olives will drop off.

Context

38Utapanda mbegu nyingi katika shamba lakini utavuna haba, kwa sababu nzige watazila. 39Utapanda mashamba ya mizabibu na kuyapalilia, lakini hutakunywa divai yake wala hutakusanya zabibu, kwa sababu wadudu watazila. 40Utakuwa na mizeituni katika nchi yako yote, lakini hutatumia hayo mafuta yake, kwa sababu zeituni zitapukutika. 41Utakuwa na wana na binti lakini hawatakuwa nawe, kwa sababu watachukuliwa mateka. 42Makundi ya nzige yatavamia miti yako yote na mazao ya nchi yako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.