Kumbukumbu 28:37
Deuteronomy 28:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utakuwa kitu cha kuchukiza, tena kitu cha kudharauliwa na kudhihakiwa kwa mataifa yote huko Bwana atakakokupeleka.
Deuteronomy 28:37 in English
Deuteronomy 28:37 · Berean Standard Bible
You will become an object of horror, scorn, and ridicule among all the nations to which the LORD will drive you.
Context
35Bwana atayapiga magoti yako na miguu yako kwa majipu yenye maumivu makali yasiyoponyeka, yakienea kutoka nyayo za miguu yako hadi utosini. 36Bwana atakupeleka wewe na mfalme uliyemweka juu yako uende kwenye taifa ambalo hukulijua wewe wala baba zako. Huko utaabudu miungu mingine, miungu ya miti na mawe. 37Utakuwa kitu cha kuchukiza, tena kitu cha kudharauliwa na kudhihakiwa kwa mataifa yote huko Bwana atakakokupeleka. 38Utapanda mbegu nyingi katika shamba lakini utavuna haba, kwa sababu nzige watazila. 39Utapanda mashamba ya mizabibu na kuyapalilia, lakini hutakunywa divai yake wala hutakusanya zabibu, kwa sababu wadudu watazila.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.