Native Bible

Deuteronomy 25:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kumbuka kile Waamaleki walichowatendea mlipokuwa njiani mkitoka Misri.

Deuteronomy 25:17 in English

Deuteronomy 25:17 · Berean Standard Bible

Remember what the Amalekites did to you along your way from Egypt,

Context

15Ni lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako. 16Kwa maana Bwana Mungu wako humchukia yeyote ambaye hufanya mambo kama haya, yeyote anayetenda kwa udanganyifu. 17Kumbuka kile Waamaleki walichowatendea mlipokuwa njiani mkitoka Misri. 18Wakati mlipokuwa mmechoka na kuishiwa nguvu kwa safari yenu, wakawapiga wale wote waliokuja nyuma. Waamaleki hawakumwogopa Mungu. 19Bwana Mungu wako atakapokupa pumziko mbali na adui zako wote wanaokuzunguka katika nchi akupayo kuimiliki kuwa urithi, utafutilia mbali kumbukumbu lote la Waamaleki chini ya mbingu. Usisahau!

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.