Kumbukumbu 23:12
Deuteronomy 23:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tengeni mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda kujisaidia.
Deuteronomy 23:12 in English
Deuteronomy 23:12 · Berean Standard Bible
You must have a place outside the camp to go and relieve yourself.
Context
10Ikiwa mtu amechafuka kwa sababu ya kutokwa na shahawa usiku, inampasa atoke nje ya kambi na kukaa huko. 11Lakini jioni ikikaribia ataoga, na baada ya jua kuzama ataingia tena kambini. 12Tengeni mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda kujisaidia. 13Kama sehemu ya vifaa vyenu kuweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho. 14Kwa kuwa Bwana Mungu wenu hutembea katika kambi yenu ili kuwalinda na kuwaweka adui zenu mikononi mwenu. Kambi yenu ni lazima iwe takatifu, ili asione kitu chochote miongoni mwenu kilicho kichafu akageuka na kuwaacha.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.