Native Bible

Deuteronomy 10:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.

Deuteronomy 10:18 in English

Deuteronomy 10:18 · Berean Standard Bible

He executes justice for the fatherless and widow, and He loves the foreigner, giving him food and clothing.

Context

16Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena. 17Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa. 18Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi. 19Nanyi wapendeni wageni, kwa kuwa ninyi wenyewe mlikuwa wageni huko Misri. 20Mche Bwana Mungu wako na umtumikie yeye. Shikamana naye kwa uthabiti na kuapa kwa jina lake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.