Kumbukumbu 10:20
Deuteronomy 10:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mche Bwana Mungu wako na umtumikie yeye. Shikamana naye kwa uthabiti na kuapa kwa jina lake.
Deuteronomy 10:20 in English
Deuteronomy 10:20 · Berean Standard Bible
You are to fear the LORD your God and serve Him. Hold fast to Him and take your oaths in His name.
Context
18Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi. 19Nanyi wapendeni wageni, kwa kuwa ninyi wenyewe mlikuwa wageni huko Misri. 20Mche Bwana Mungu wako na umtumikie yeye. Shikamana naye kwa uthabiti na kuapa kwa jina lake. 21Yeye ni sifa yako; yeye ni Mungu wako, ambaye alikutendea yale maajabu makubwa na ya kutisha uliyoyaona kwa macho yako mwenyewe. 22Baba zako walioshuka kwenda Misri jumla yao walikuwa sabini, na sasa Bwana Mungu wako amekufanya wengi kama nyota za angani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.