Kumbukumbu 10:16
Deuteronomy 10:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena.
Deuteronomy 10:16 in English
Deuteronomy 10:16 · Berean Standard Bible
Circumcise your hearts, therefore, and stiffen your necks no more.
Context
14Mbingu, hata mbingu za juu sana, dunia na kila kitu kilichomo ndani yake, ni mali ya Bwana Mungu wako. 15Hata hivyo Bwana alikuwa na shauku na baba zako, akawapenda na akawachagua ninyi, wazao wao, kuliko mataifa yote, kama ilivyo leo. 16Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena. 17Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa. 18Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.