Native Bible

Daniel 5:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa: mene, mene, tekeli na peresi

Daniel 5:25 in English

Daniel 5:25 · Berean Standard Bible

Now this is the inscription that was written: MENE, MENE, TEKEL, PARSIN.

Context

23Badala yake, umejiinua dhidi ya Bwana wa mbingu. Uliletewa vikombe vya Hekalu lake, nawe na wakuu wako, wake zako na masuria wako mlivitumia kwa kunywea mvinyo. Ukaisifu miungu ya fedha na dhahabu, ya shaba, chuma, miti na mawe, miungu ambayo haiwezi kuona, au kusikia wala kufahamu. Lakini hukumheshimu Mungu ambaye anaushikilia uhai wako na njia zako zote mkononi mwake. 24Kwa hiyo ameutuma mkono ule ulioandika maneno. 25“Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa: mene, mene, tekeli na peresi 26“Hii ndiyo maana ya maneno haya: “Mene: Mungu amezihesabu siku za utawala wako na kuukomesha. 27Tekeli : Wewe umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.