Amosi 9:10
Amos 9:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watenda dhambi wote miongoni mwa watu wangu watauawa kwa upanga, wale wote wasemao, ‘Maafa hayatatupata wala kutukuta.’
Amos 9:10 in English
Amos 9:10 · Berean Standard Bible
All the sinners among My people will die by the sword— all those who say, ‘Disaster will never draw near or confront us.’”
Context
8“Hakika macho ya Bwana Mwenyezi
yako juu ya ufalme wenye dhambi.
Nami nitauangamiza
kutoka kwenye uso wa dunia:
hata hivyo sitaiangamiza kabisa
nyumba ya Yakobo,”
asema Bwana. 9“Kwa kuwa nitatoa amri,
na nitaipepeta nyumba ya Israeli
miongoni mwa mataifa yote,
kama vile nafaka ipepetwavyo katika ungo,
na hakuna hata punje moja itakayoanguka chini. 10Watenda dhambi wote miongoni mwa watu wangu
watauawa kwa upanga,
wale wote wasemao,
‘Maafa hayatatupata wala kutukuta.’ 11“Katika siku ile nitaisimamisha
hema ya Daudi iliyoanguka.
Nitakarabati mahali palipobomoka
na kujenga upya magofu yake,
na kuijenga kama ilivyokuwa awali, 12ili wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu,
na mataifa yote yale yanayobeba Jina langu,”
asema Bwana ambaye atafanya mambo haya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.