Amosi 9:12
Amos 9:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
ili wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote yale yanayobeba Jina langu,” asema Bwana ambaye atafanya mambo haya.
Amos 9:12 in English
Amos 9:12 · Berean Standard Bible
that they may possess the remnant of Edom and all the nations that bear My name,”* declares the LORD, who will do this.
Context
10Watenda dhambi wote miongoni mwa watu wangu
watauawa kwa upanga,
wale wote wasemao,
‘Maafa hayatatupata wala kutukuta.’ 11“Katika siku ile nitaisimamisha
hema ya Daudi iliyoanguka.
Nitakarabati mahali palipobomoka
na kujenga upya magofu yake,
na kuijenga kama ilivyokuwa awali, 12ili wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu,
na mataifa yote yale yanayobeba Jina langu,”
asema Bwana ambaye atafanya mambo haya. 13“Siku zinakuja,” asema Bwana,
“wakati mvunaji atatanguliwa na mkulima,
naye mpanzi atatanguliwa na yeye akamuaye zabibu.
Divai mpya itadondoka kutoka milimani,
na kutiririka kutoka vilima vyote. 14Nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa;
wataijenga tena miji iliyoachwa magofu,
nao wataishi ndani mwake.
Watapanda mizabibu na kunywa divai yake;
watalima bustani na kula matunda yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.