Amosi 5:6
Amos 5:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtafuteni Bwana mpate kuishi, au atafagia nyumba ya Yosefu kama moto; utawateketeza, nayo Betheli haitakuwa na yeyote wa kuuzima.
Amos 5:6 in English
Amos 5:6 · Berean Standard Bible
Seek the LORD and live, or He will sweep like fire through the house of Joseph; it will devour everything, with no one at Bethel to extinguish it.
Context
4Hili ndilo Bwana asemalo kwa nyumba ya Israeli:
“Nitafuteni mpate kuishi; 5msitafute Betheli,
msiende Gilgali,
msisafiri kwenda Beer-Sheba.
Kwa maana kwa hakika Gilgali itakwenda uhamishoni,
na Betheli itafanywa kuwa si kitu.”* 6Mtafuteni Bwana mpate kuishi,
au atafagia nyumba ya Yosefu kama moto;
utawateketeza, nayo Betheli
haitakuwa na yeyote wa kuuzima. 7Ninyi ambao mnageuza haki kuwa uchungu
na kuiangusha haki chini 8(yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni,
ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko
na mchana kuwa usiku,
ambaye huyaita maji ya bahari
na kuyamwaga juu ya uso wa nchi:
Bwana ndilo jina lake;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.