Native Bible

Amos 5:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hili ndilo Bwana asemalo kwa nyumba ya Israeli: “Nitafuteni mpate kuishi;

Amos 5:4 in English

Amos 5:4 · Berean Standard Bible

For this is what the LORD says to the house of Israel: “Seek Me and live!

Context

2“Bikira Israeli ameanguka, kamwe hatainuka tena, ameachwa pweke katika nchi yake, hakuna yeyote wa kumwinua.” 3Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “Wakati mmoja wa miji yako utakapopeleka watu elfu moja vitani kwa ajili ya Israeli, mia moja tu watarudi; wakati mji utakapopeleka mia moja, kumi tu ndio watarudi hai.” 4Hili ndilo Bwana asemalo kwa nyumba ya Israeli: “Nitafuteni mpate kuishi; 5msitafute Betheli, msiende Gilgali, msisafiri kwenda Beer-Sheba. Kwa maana kwa hakika Gilgali itakwenda uhamishoni, na Betheli itafanywa kuwa si kitu.”* 6Mtafuteni Bwana mpate kuishi, au atafagia nyumba ya Yosefu kama moto; utawateketeza, nayo Betheli haitakuwa na yeyote wa kuuzima.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.