Amosi 5:13
Amos 5:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo mtu mwenye busara hunyamaza kimya nyakati kama hizo, kwa kuwa nyakati ni mbaya.
Amos 5:13 in English
Amos 5:13 · Berean Standard Bible
Therefore, the prudent keep silent in such times, for the days are evil.
Context
11Mnamgandamiza maskini
na kumlazimisha awape nafaka.
Kwa hiyo, ingawa mmejenga majumba ya mawe ya fahari,
hamtaishi ndani yake;
ingawa mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu,
hamtakunywa divai yake. 12Kwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu
na ukubwa wa dhambi zenu.
Mmewaonea wenye haki na kupokea rushwa
na kuzuia haki ya maskini mahakamani. 13Kwa hiyo mtu mwenye busara hunyamaza kimya nyakati kama hizo,
kwa kuwa nyakati ni mbaya. 14Tafuteni mema, wala si mabaya,
ili mpate kuishi.
Ndipo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote atakuwa pamoja nanyi,
kama msemavyo yupo nanyi. 15Yachukieni maovu, yapendeni mema;
dumisheni haki mahakamani.
Yamkini Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote
atawahurumia mabaki ya Yosefu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.