Amosi 5:15
Amos 5:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yachukieni maovu, yapendeni mema; dumisheni haki mahakamani. Yamkini Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote atawahurumia mabaki ya Yosefu.
Amos 5:15 in English
Amos 5:15 · Berean Standard Bible
Hate evil and love good; establish justice in the gate. Perhaps the LORD, the God of Hosts, will be gracious to the remnant of Joseph.”
Context
13Kwa hiyo mtu mwenye busara hunyamaza kimya nyakati kama hizo,
kwa kuwa nyakati ni mbaya. 14Tafuteni mema, wala si mabaya,
ili mpate kuishi.
Ndipo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote atakuwa pamoja nanyi,
kama msemavyo yupo nanyi. 15Yachukieni maovu, yapendeni mema;
dumisheni haki mahakamani.
Yamkini Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote
atawahurumia mabaki ya Yosefu. 16Kwa hiyo hili ndilo Bwana, Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, asemalo:
“Kutakuwepo maombolezo katika barabara zote
na vilio vya uchungu katika njia kuu zote.
Wakulima wataitwa kuja kulia,
na waombolezaji waje kuomboleza. 17Kutakuwepo kuomboleza katika mashamba yote ya mizabibu,
kwa kuwa nitapita katikati yenu,”
asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.