Amosi 1:4
Amos 1:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitatuma moto juu ya nyumba ya Hazaeli ambao utateketeza ngome za Ben-Hadadi.
Amos 1:4 in English
Amos 1:4 · Berean Standard Bible
So I will send fire upon the house of Hazael to consume the citadels of Ben-hadad.
Context
2Alisema:
“Bwana ananguruma toka Sayuni,
pia ananguruma kutoka Yerusalemu;
malisho ya wachunga wanyama yanakauka,
kilele cha Karmeli kinanyauka.” 3Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kwa dhambi tatu za Dameski,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu aliipura Gileadi
kwa vyombo vya chuma vyenye meno. 4Nitatuma moto juu ya nyumba ya Hazaeli
ambao utateketeza ngome za Ben-Hadadi. 5Nitalivunja lango la Dameski;
nitamwangamiza mfalme aliyeko katika Bonde la Aveni,*
na yeye ambaye anaishika fimbo ya utawala katika Beth-Edeni.
Watu wote wa Aramu watakwenda uhamishoni huko Kiri,”
asema Bwana. 6Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kwa dhambi tatu za Gaza,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu walichukua mateka jumuiya nzima
na kuwauza kwa Edomu,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.