Matendo 9:7
Acts 9:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu waliokuwa wakisafiri pamoja na Sauli wakasimama bila kuwa na la kusema, kwa sababu walisikia sauti lakini hawakumwona aliyekuwa akizungumza.
Acts 9:7 in English
Acts 9:7 · Berean Standard Bible
The men traveling with Saul stood there speechless. They heard the voice but did not see anyone.
Context
5Sauli akajibu, “U nani wewe, Bwana?”
Ile sauti ikajibu, “Mimi ni Yesu unayemtesa. 6Sasa inuka uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.” 7Watu waliokuwa wakisafiri pamoja na Sauli wakasimama bila kuwa na la kusema, kwa sababu walisikia sauti lakini hawakumwona aliyekuwa akizungumza. 8Sauli akainuka kutoka pale chini na alipojaribu kufungua macho yake hakuweza kuona kitu chochote. Basi wakamshika mkono wakamwongoza mpaka Dameski. 9Naye kwa muda wa siku tatu alikuwa kipofu naye hakula wala kunywa chochote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.