Matendo 9:8
Acts 9:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sauli akainuka kutoka pale chini na alipojaribu kufungua macho yake hakuweza kuona kitu chochote. Basi wakamshika mkono wakamwongoza mpaka Dameski.
Acts 9:8 in English
Acts 9:8 · Berean Standard Bible
Saul got up from the ground, but when he opened his eyes he could not see a thing.* So they led him by the hand into Damascus.
Context
6Sasa inuka uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.” 7Watu waliokuwa wakisafiri pamoja na Sauli wakasimama bila kuwa na la kusema, kwa sababu walisikia sauti lakini hawakumwona aliyekuwa akizungumza. 8Sauli akainuka kutoka pale chini na alipojaribu kufungua macho yake hakuweza kuona kitu chochote. Basi wakamshika mkono wakamwongoza mpaka Dameski. 9Naye kwa muda wa siku tatu alikuwa kipofu naye hakula wala kunywa chochote. 10Huko Dameski alikuwepo mwanafunzi mmoja jina lake Anania. Bwana alimwita katika maono, “Anania!”
Akajibu, “Mimi hapa Bwana.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.