Matendo 8:4
Acts 8:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo wale waliotawanyika wakalihubiri neno la Mungu kila mahali walipokwenda.
Acts 8:4 in English
Acts 8:4 · Berean Standard Bible
Those who had been scattered preached the word wherever they went.
Context
2(1) Siku ile kukatukia mateso makuu dhidi ya kanisa huko Yerusalemu, waumini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia Uyahudi na Samaria. (2) Watu wacha Mungu wakamzika Stefano na kumwombolezea sana. 3Lakini kwa habari ya Sauli alikuwa analiharibu kanisa, akiingia nyumba kwa nyumba, akiwaburuta wanawake na wanaume na kuwatupa gerezani. 4Kwa hiyo wale waliotawanyika wakalihubiri neno la Mungu kila mahali walipokwenda. 5Filipo akateremkia mji mmoja wa Samaria akawahubiria habari za Kristo* 6Watu walipomsikia Filipo na kuona ishara na miujiza aliyofanya, wakasikiliza kwa bidii yale aliyosema.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.