Matendo 2:31
Acts 2:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Daudi, akiona mambo yaliyoko mbele, akanena juu ya kufufuka kwa Kristo,* kwamba hakuachwa kaburini, wala mwili wake haukuona uharibifu.
Acts 2:31 in English
Acts 2:31 · Berean Standard Bible
Foreseeing this, David spoke about the resurrection of the Christ, that He was not abandoned to Hades, nor did His body see decay.
Context
29“Ndugu zangu Waisraeli, nataka niwaambie kwa uhakika kwamba baba yetu Daudi alikufa na kuzikwa, nalo kaburi lake lipo hapa mpaka leo. 30Lakini alikuwa nabii na alijua ya kuwa Mungu alikuwa amemwahidi kwa kiapo kwamba angemweka mmoja wa wazao wake penye kiti chake cha enzi. 31Daudi, akiona mambo yaliyoko mbele, akanena juu ya kufufuka kwa Kristo,* kwamba hakuachwa kaburini, wala mwili wake haukuona uharibifu. 32Mungu alimfufua huyu Yesu na sisi sote ni mashahidi wa jambo hilo. 33Basi ikiwa yeye ametukuzwa kwa mkono wa kuume wa Mungu, amepokea kutoka kwa Baba ahadi ya Roho Mtakatifu, naye amemimina kile mnachoona sasa na kusikia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.